Waziri wa mazingira huko Burundi
Emmanuel Niyonkuru, amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura
saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.
Police wanasema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero .
Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria
kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali.
Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.
Source BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment