Monday, January 2, 2017

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Todd Whitman ahofia wajukuu zake chini ya uongozi wa Donald Trump
Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza
ripoti za sayansi.
Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini.
Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara.
Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira.
Rais mteule Donald Trump wa Marekani

Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic.
Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na kuvunjilia mbali idara ya kawi nchini Marekani pamoja na EPA.
Source BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment