Kampuni ya muziki ya Sony imemuomba
radhi mwanamuziki nyota wa pop Britney Spears, baada ya ukurasa wake
rasmi kutangaza kuwa amefariki.
Kampuni hiyo ya burudani iliondoa
mara moja ujumbe wake batili, ikisema kuwa akaunti yake ilikuwa
"imedukuliwa" lakini kwamba hali hiyo "imerekebishwa.Sony iliongeza kusema kuwa '' samahani kwa Britney Spears na mashabiki wake kwa mkanganyiko wowote uliojitokeza".
Britney Spears mwenye umri wa miaka 35 hakujibu moja kwa moja kupitia mtandao wake wa Twitter, lakini meneja wake amethibitisha kuwa muimbaji huyo yuko ''salama salmini''.
Hali kadhalika Ukurasa wa Twitter rasmi wa afisa wa Sony Bob Dylan pia ulionekana kudukuliwa.
Ulitumwa ujumbe uliosema: "pumzika kwa amani @britneyspears" katika muda sawa na ule uliotumwa ujumbe bandia wa Sony.
Haijabainika wazi iwapo ndiyo iliyohusika katika utumaji wa jumbe za uongo au la.
Siku chache zilizopita, ilionekana kuingilia akaunti ya Twitter ya Netflix nchini Marekani na ile ya Marvel Entertainment.
Pia ilihusishwa na udukuzi wa akaunti ya Twitter ya wakurugenzi wakuu akiwemo mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg na mkurugenzi mkuu wa Google Sundar Pichai.
Source BBC swahili
0 comments:
Post a Comment