Rais mteule wa Marekani Donald
Trump, amemtaja mkosoaji mkubwa wa biashara za Kichina Peter Navarro
kuwa kiongozi mkuu wa baraza jipya la kibiashara katika Ikulu ya White
House.
Peter Navarro, alizindua sera ngumu dhidi ya Beijing na
akaandika kitabu kwa jina "Death by China: How America Lost its
Manufacturing Base". Yani kifo cha China: namna Marekani ilipopoteza
uwezo wake wa uundaji bidhaa" Serikali ya mpito ya Doland Trump, imemsifu kwa uwezo wake wa kufufua uchumi, mbali na kukabiliana na uhaba wa kazi kwa Wamarekani.
Bwana Trump pia, ameteua mwekezaji bilionea na msomi wa uchumi, Carl Icahn, kama mshauri mkuu wa mageuzi.
Bw Icahn, amesema kuwa biashara nchini Marekani, imelemazwa na masharti mengi yasio na maana.
0 comments:
Post a Comment