Monday, January 2, 2017

Islamic State lakiri kutekeleza shambulio Istanbul

Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio la kilabu ya usikju mjini Istanbul
Kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio baya dhidi ya watu waliokuwa wakiukaribisha mwaka mpya wa 2017 katika klabu moja ya usiku mjini Istanbul Uturuki.
Katika taarifa, kundi hilo limemtaja muuaji aliyekuwa na bunduki ya rashasha kama shujaa wa kundi hilo.
Huku Polisi wa Uturuki wakiendelea kumsaka mshukiwa huyo mkuu aliyetekeleza shambulio hilo, taarifa za kina zimefichua kuhusu shambulio hilo.
Vyombo vya habari nchini Uturuki vinasema kuwa, muuaji huyo aliwasili katika clabu hiyo kwa kutumia texi, kabla ya kuwapiga walinzi wawili risasi na kuwauwa papo hapo, kabla ya kuingia ndani ya klabu hiyo ya burudani na kuanza kuwamiminia
risasi kiholela watu waliokuwa katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya.
Inasemekana aliwamiminia watu risasi zaidi ya 180 kwa muda wa dakika saba.
Alibadilisha jaketi lake na kisha akatoweka ndani ya umati uliookuwa umejawa na taharuki.
Watu 25 kati ya waliouwawa, walikuwa raia wa kigeni, wengi wao kutoka mashariki ya kati na kaskazini mwa bara Afrika, wakiwemo raia wa Saudi Arabia.
Source BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment