Monday, January 2, 2017

Aliyeweka nyama ya nguruwe msikitini afariki

Kevin aliweka vipande vya nyama ya nguruwe katika mlango wa msikiti wa Jamia huko Totterdown

Mtu aliyeweka nyama ya nguruwe katika mlango wa msikiti nchini Uingereza amefariki akihudumia kifungo cha miezi 12 jela.
Kevin Crehan alihukumiwa kifungo hicho katika mahakama ya Bristol Crown mnamo mwezi Julai kwa kuchochea machafuko ya uma.
Vipande vya nyama ya nguruwe viliwekwa katika mlango wa msikiti wa Jamia huko Totterdown.
Msemaji wa hudumu za jela hiyo amethibitisha kuwa Kevin mwenye umri wa miaka 35 alifariki siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa uchunguzi unaendelea.
Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.
Jela hiyo imekataa kutoa maelezo yoyote ya sababu ya kifo chake.
Source BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment