Monday, January 2, 2017

Mshambuliaji wa Istanbul alifyatua risasi 180

Mshambuliaji wa mkahawa wa Istanbul anaendelea kusakwa
Huku polisi wa Uturuki wakiwa katika harakati za kumsaka mtu aliyetekeleza shambulio katika kilabu moja ya burudani huko mjini Istanbul na kuwauwa watu 39, taarifa za kina zimefichuka kuhusu shambulio hilo.
Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa shambulio hilo lilidumu kwa dakika 7.
Kuna ushahidi unaonesha kuwa mshambuliaji alifika eneo hilo akitumia usafiri wa teksi.

Alikuwa na mzigo ambao huenda ndio bunduki aliyoitumia aina ya automatic rifle.
Punde tu alipofika kwenye klabu hicho, aliwapiga risasi walinzi wawili na kisha kuingia ndani huku akiendelea kuwafyatulia risasi watu waliokuwa wamejaa sehemu hiyo kusherehekea ujio wa mwaka mpya.
Kisha mtu huyo akatumia vurugu alizozisababisha kugeuza nguo na kutoroka.
Maafisa wa polisi wanamsaka mshambuliaji huku raia wa mji huo wakindelea kuomboleza

Kati ya 25 waliofariki ni raia wa mataifa ya kigeni wakiwemo kutoka Israel, Urusi , Ufaransa , Tunisia, Lebanon, India, Ubelgiji, Jordan ,Canada na na raia watan wa Saudia.
Lengo la shambulio hilo bado halijulikani ,lakini kuna tuhuma kwamba huenda kundi la Islamic State ndilo lililotekeleza shambulio hilo kwa kuwa lilihusishwa na mashambulio mawili ya ugaidi nchini humo mwaka uliopita.
Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa kundi hilo lilijaribu kuzua ghasia.
Chama kilichopigwa marafuku cha Kurdistan Workers Party PKK kimejitenga na shambulio hilo kikisema hakiwezi kuwalenga raia wasio na hatia.
Awali ,waziri wa maswala ndani nchini humo Suleyman Soylu alithibitisha kwamba usakaji wa muuaji huyo unaendelea .
Maafisa wa polisi wamezindua operesheni.Tunatumai mshambuliaji huyo atakamatwa hivi karibuni.
Lakini huku shughuli ya kumsaka mtu huyo ikiendelea, mazishi ya wale waliouawa katika kilabu hicho yameanza kufanyika.

0 comments:

Post a Comment