Polisi huko Canada wamemkamata
rubani mmoja aliyepatikana ,ndani ya ndege ya abiria kwenye chumba cha
marubani akiwa amelewa chakari kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa.
Rubani
huyo alikuwa amepangiwa kuendesha ndege hiyo kwa safari ya kutoka
uwanja wa ndege wa Calgary Canada hadi nchini Mexico ndipo lakini
wafanyikazi wenzake wakamuona hakuwa katika hali sawa na kupiga ripoti.Kisha punde baadae akaanguka na kuzirai.
Sasa amezindukia mashtaka ya kutaka kuendesha ndege akiwa mlevi na utovu wa nidhamu kazini.
Baadae rubani mwengine aliendesha ndege hiyo ya shirika liitwalo Sunwing iliyokuwa inaelekea Cancun mjini Mexico, ikiwa na abiria zaidi ya 100.
0 comments:
Post a Comment