Habari kutoka mji mkuu wa Somalia,
zasema kuwa watu wanne wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya
mlipuaji wa kujitoa kufa alipojilipua karibu na uwanja wa ndege mjini
Mogadishu.
Idara ya Polisi imesema kuwa, mhanga huyoaliyevalia vilipuzi na kuweka mabomu ndani ya gari alilokuwa akiliendesha, alilipua bomu hilo katika kizuizi chya barabarani mita chache karibu na uwanja wa ndege wa Somalia mjini Mogadishu.
Kapteni Mohamed Hussein amesema kuwa walinda usalama walikuwa wakilipekuwa gari hilo ndipo likalipuka mita 100 kutoka makao makuu ya majeshi ya muungano wa Afrika ya kulinda amani AMISOM. Pia eneo hilo ni karibu na Hoteli ya amani.
Source BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment