Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? ungefunga ndoa na roboti? na Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?
Haya
ni baadhi ya maswala machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa
kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika chuo kikuu
cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio
iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina .Hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.
Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.
Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono.
''Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya''.
Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema.
Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.
Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.
Source BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment