Monday, January 2, 2017

Watu 39 wauawa wakikaribisha mwaka mpya Uturuki

Mshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa

Takriban watu 39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.
Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.
Muuaji wa watu 39 katika kilabu
ya burudani Uturuki asakwa
Urusi na Marekani zalaani shambulio Uturuki
Waziri huyo Süleyman Soylu ameelezea waliojeruhiwa kuwa 69 .
Kulingana na waziri wa maswala ya ndani takriban watu 39 wamefariki huku 69 wakijeruhiwa
Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.
Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.
Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.
Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.   
Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.
Source BBC Swahili 

0 comments:

Post a Comment