Waandamanaji watatu wameuawa na wanajeshi katika mji mkuu wa DR Congo Kinshasa ,kulingana na mtandao wa polico.cd nchini humo.
Watu
wengine watano walijeruhiwa, wawili vibaya baada ya kupigwa risasi
wakiwa karibu na maafisa wa kikosi cha Republican Guard katika mji wa
N'djili mojawapo ya wilaya zenye idadi kubwa ya watu.
DR Congo imo kwenye 'hatari kubwa'
Kabila: Sitowania urais tena
Kundi la upinzani lamtaka Kabila kujiuzulu
Maandamano ya kumtaka Kabila kujiuzulu yafanyika duniani
Milio ya risasi bado inaendelea kusikika katika maeneo tofauti mji Kinshasa, licha ya kuwa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi ametaka kufanyika kwa maandamano ya amani, ripoti hiyo imeongezea.
Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji kadhaa ya DR Congo ambapo muhula wa rais Joseph Kabila uliisha siku ya Jumatatu.
Wakati huohuo kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.
Mapema siku ya Jumanne milio ya risasi iliendelea kusikika huku waandamanaji wakimtaka rais Kabila kujiuzulu.
Raia bado wanaendelea kupiga firimbi mjini Kinshasa.
Wanasema kuwa hatua hiyo inatoa ishara kwamba muhula wa Kabila umekamilika.
Pia wanaimba kwamba Kabila Must Go { kabila ni sharti aondoke mamlakani}, kulingana na ripoti za BBC
Source BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment