|
Mji wa Dar es Salaam nchini Tanzania
|
Viwango vya wanawake kuweza kupata
mimba nchini Tanzania vimepungua hadi 5.2 kwa kila mwanamke nchini
Tanzania mwaka 2015/2016 kutoka 6.2 kwa kila mwanamke miaka ya
1991/92, kulingana na utafiti wa afya nchini humo
Kulingana na
gazeti la The Citizen nchini Tanzania,utafiti huo uliofanywa na
kutolewa na Afisi ya kitaifa ya Takwimu nchini humo NBS wiki iliopita
unaonyesha kushuka kwa viwango vya uwezo wa kushika mimba miongoni mwa
wanawake .
Kwa mfano mwaka 1996 ripoti hiyo inaonyesha watoto 5.8, mwaka 2004/05} ni watoto 5.7 mwaka 2010 ni watoto 5.4.
Utafiti
huo pia ulibaini kwamba wanawake wanaoishi mashambani nchini humo wana
uwezo mkubwa wa kushika mimba ikilinganishwa na wenzao wanaoishi mijini.
Gazeti hilo linasema kuwa wanawake wa mashambani wana uwezo wa
kupata watoto 6 kwa kiwango cha wastani ikilinganishwa na wenzao wa
mijini walio na uwezo wa kupata watoto watatu kwa wastani.